Baada ya mchekshaji Ebitoke kujitokeza hadaharani akimtaka kimapenzi mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ben Pol hatimaye ombi lake limetimia.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Ben Pol leo ameweka picha za mahaba akiwa pamoja na mchekeshaji huyo ambapo wamewaacha watu midomo wazi kama kweli washaingia kwenye mahusiano ama kiki tu.

Ben Pol ameweka picha akiwa na Ebitoke na kuweka maneno ambayo yanaelezea hisia zake pia kwa kilichofanywa na mchekeshaji huyo kwa kuheshimu hisia zake.

Ameandika kuwa “Hakuna kitu kizuri kama kujishusha na kukubali kujifunza pale unapoona kuna jambo zuri la Kujifunza. Ikiwa unampenda mtu Au unatamani nafasi fulani, utajuaje kama unaweza kuipata hiyo nafasi au la Ikiwa haujaiomba kwa Mhusika?

Pia ameongeza kwa kuandika “Naamini watu wengi sana wameoa ama kuolewa na watu wasiowapenda kwa sababu tu walipoteza nafasi za kuwaambia hisia zao wale Wawapendao, Mwishowe walipokuwa tayari kuwaambia, ikawa Too late. Ikumbukwe humu duniani sisi sote TUNAPITA, labda huyo Mtu kesho hatokuwepo.

Wawili hao hadi sasa wamewacha mashabiki wao midomo wazi wakijiuliza je wameanza kwenye mahusiano au ni kiki tu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *