Mwanamuziki nyota wa RnB nchini, Ben Pol amesema kuwa yeye ndio msanii pekee aliyesababisha show za muziki wa RnB kufanyika uwanjani tofauti na zamani zilikuwa zikifanyika ukumbini pekee.
Muimbaji huyo amesema kuwa hapo mwanzo watu walizoea kuwaona wasanii wa RnB wakifanya show ukumbini tu.
Pia Ben Pol amesema lakini kama atokuwa msanii wa kwanza kufanya hivyo basi atakuwa ni miongoni mwa wasasnii waliofanya hilo likawezekana.
Ben ameongeza kuwa atahakikisha anaachia kazi yake mpya siku si nyingi kwa ajili ya kufunga mwaka na kuanza mwaka vizuri.
Mwanamuziki huyo amefanikiwa kufanya show za Fiesta katika mikoa mbali mbali na kuhitimishwa jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Leaders.