Mwanaumziki nyota wa Bongo fleva, Ben Paul amesema kuwa amefurahishwa na mafanikio aliyoyapata katika onesho lake alilolifanya Offenbach nchini Ujerumani mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julisu Nyerere akitokea Ujerumani jana, Paul alisema amepata mafanikio makubwa katika onesho hilo kwani amepata mashabiki ambao hakuwatarajia.

Pia amesema kuwa  hayo ni mafanikio makubwa kwake hasa kwa vile aliimba ‘live’ katika nchi iliyo nje ya Afrika.

Alisema katika onesho hilo Mwafrika alikuwa peke yake na akitumbuiza ‘live’ wimbo wake wa Moyo Mashine, Wajerumani walionekana kuufurahia.

Alisema watu takriban 10,000 walihudhuria onesho hilo na limeacha historia katika maisha yake.

Vile vile Ben Pol amesema kuwa katika maisha yake ya kimuziki onesho hilo ni la tatu kupata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki, ikiwa ni pamoja na onesho la Fiesta lililofanyika Dodoma.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *