Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ben Pol amefunguka kuhusu wasanii kutoa albamu lakini wanakuwa wasiri katika mauzo na idadi kamili ya copy.

Ben Pol amesema kuwa ni kweli hilo lipo ila kwa upande wake hadhani kama lipo kutokana albamu yake ya kwanza alitoa akiwa chini ya record label.

“Albamu ya kwanza ilikuwa chini ya record label ‘M Lab’ kwa hiyo hao ndio walifanya makubaliano na distributor na wakafunga hiyo dili, mimi nilikuwa na kati yangu kidogo tu kutokana na nilivyosaini nilivyoanza kufanya kazi na ile label, kwa hiyo ni ngumu sana kujua mauzo ya ile albamu” amesema.

“Hii ya sasa hivi (The Best of Ben Pol) executive producer ni mimi mwenyewe, kwa hiyo wale producer 15 unaowaona mimi ni boss wao naweza nikasema maana niliongea nao nikafanya payment kama ni nyimbo tatu au mbili, na production ya CD na vitu vyote nimeingia gharama” ameongeza.

Hadi kufikia sasa Ben Pol ana albamu mbili katika muziki wa Bongo Flava, Maboma ilikuwa albamu ya kwanza na The Best of Ben Pol ambayo imetoka hivi karibuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *