Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ben Pol amesema kuwa kitu pekee anachokiangalia na kumvutia kwa mwanamke ambaye ataweza kumzimikia na kuwa naye kimapenzi ni lazima awe anajiamini pindi wakiwa wanaongea au hata wakiwa wana-chat.

Ben Pol amefunguka hayo baada ya kupita siku chache tokea aliyekuwa anadaiwa kutoka naye kimapenzi ambaye ni msanii wa vichekesho nchini Anastazia Kisaveli ‘Ebitoke’ kulalamika kwamba hapokelewi simu yake wala kujibiwa ujumbe mfupi pindi amtumiapo Ben.

“Endapo nikimpenda msichana sifa kubwa huwa naangalia ‘confidence’ yake pindi tukiwa tunaongea na ku-chat, U-smart, umakini na uharaka katika kujibu vitu ambavyo anaulizwa kwa wakati huo”, amesema Ben Pol.

Ben Pol kwa sasa anatamba na kazi yake mpya iliyopewa jina la ‘Kidume’ ambaye amemshirikisha msanii kutoka Nigeria anayejulikana kwa jina la Chidinma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *