Staa wa filamu za Batman, Ben Affleck ameondolewa kwenye jukumu la kuongoza filamu mpya ya Batman baada ya kupewa jukumu la kuigiza kwenye filamu hiyo.

Kampuni ya kutengeneza filamu ya Warner Bros inayosimamia filamu hiyo imetoa taarifa ya kutafuta muongozaji mpya wa filamu hiyo kuchukua nafasi ya Affleck.

‘Ni wazi kuwa siwezi kufanya kazi zote mbili kwa kiwango ambacho Warner Bros wanakihitaji’.

‘Kuna baadhi ya wahusika kwenye filamu huwa na mvuto maalum kwenye mioyo ya mamilioni ya mashabiki. Kufanya kazi hiyo hadi mashabiki wakupende kunahitaji kujitoa na kuelekeza kila kitu chako kwenye eneo hilo na kwenye mioyo ya watu’.

Ben Affleck alianza kuwa nyota wa kampuni ya Warner Bros mwaka jana alipocheza filamu ya Batman v Superman: Dawn of Justice, ambayo hata hivyo ilikuwa na mapokeo mchanganyiko kutoka kwa mashabiki.

Bado haijafahamika filamu hiyo ambayo bado haijapewa jina itatoka mwaka gani lakini inadhaniwa kuwa mwaka 2018 ndio mwaka itakapoachiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *