Belle 9 amesema kuwa pamoja na mashabiki kuponda mtindo wake mpya wa nywele (bleach) amejifunza kuwa anaangaliwa sana na kila anachokifanya kina impact kubwa kwa mashabiki wake.

Amedai kuwa licha ya kupata mrejesho hasi, hajisikii vibaya kwakuwa yeye ni mtu anayependa fashion na kuwa tofauti mara zote. Muimbaji huyo ameongeza kuwa kama msanii amekuwa akijitahidi kuwa tofauti kila mara huku akiwatolea mfano wasanii wa nje akiwemo Chris Brown kuwa nao wamekuwa wakifanya hivyo.

Belle ambaye anatarajia kuachia remix ya wimbo wake Bulger Movie Selfie (BMS), amesema watu wasishangae baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhan akaja tena na mtindo mpya wa nywele.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *