Staa wa miondoko ya dansi nchini, Christian Bella amezungumzia sababu zinazomfanya aweze kumsimamia mwanamuziki mwingine huku akisisitiza ni lazima awe na uwezo wa kuimba.

Staa huyo amesema msanii anayemsimamia anataka awe na uwezo mzuri ili akitoa kazi ifanikiwe na isipofanikiwa hataweza kukaa na mtu ambaye hawezi kazi na asiye na nyota.

Bella amesema kwamba hapendi kuona msanii wake anayeimba na yeye akafanye collabo au aimbe nyimbo tatu au nne zikafeli inaonekana kama yeye anahifadhi mtu ambaye hana nyota.

Christian Bella & Malaika Band - Amerudi

Staa huyo ameongeza kwa kusema msanii ambaye yuko naye anataka akitoa nyimbo yake ya kwanza akitambulisha ifanye vizuri na ikifeli atamwambia afanye nyingine ikishindika basi anakata nae mkataba kwa kuwa uhenda hana nyota.

Christian bella pia amesema kwamba iwapo msanii huyo atafanya poa basi hata yeye mwenyewe ataweka nguvu zake kumsapoti ili mradi aweze kufanya vizuri katika soko la muziki hapa nchini.

Mwanamuziki huyo kwasasa anatamba na nyimbo yake inayojulikana kwa jina la “Nishike” ambapo inafanya vizuri katika vituo mbali mbali vya runinga na radio mpaka kumpelekea msanii huyo kupata show tofauti nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *