Beki wa zamani wa timu ya taifa ya England na Aston Villa, Ugo Ehiogu amefariki dunia baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo jana.

Ehiogu alipatwa na mshtuko wa moyo akiwa katika kituo cha mazoezi cha klabu ya Tottenham Hotspur.

Taarifa ya Spurs ilsiema Ehiogu alifariki mapema leo siku ya Ijumaa akiwa hospitalini alipokuwa anatibiwa.

Ehiogu, ambaye alikuwa kocha wa timu ya Spurs ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23, alikuwa amechezea timu ya taifa ya England mechi nne na kufunga bao moja.

Ehiogu alichezea Atson Villa karibu mechi 200 kati ya 1991 na 2000 kisha akacheza miaka saba Middlesbrough.

Alishinda Kombe la Ligi akiwa na Villa mwaka 1994 na 1996 na pia akiwa na Boro mwaka 2004.

Beki huyo pia alichezea West Brom, Leeds, Rangers na Sheffield United, kabla ya kustaafu 2009.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *