Beki wa klabu ya Paris Saint-Germain kutoka Ivory Coast, Serge Aurier amesifiwa baada yake kuokoa maisha ya mchezaji wa Mali Moussa Doumbia Jumamosi

Doumbia alianguka na kupoteza fahamu baada ya kukabwa na Lamine Kone wa Sunderland.

Aurier aliingia kati baada ya kuona mchezaji huyo wa Rostov alikuwa anakaribia akamlaza kwa upande na kumzuia kuumeza ulimi wake.

Meneja wa Mali Alain Giresse amesema alizungumza na Aurier baada ya mchezo huo na kumshukuru.

Wachezaji wote waligundua kwamba Doumbia alikuwa anakabwa kooni na kushindwa kupumua na alikuwa karibu kuumeza ulimi wake.

Katika mechi hiyo Ivory Coast ilishinda 3-1 katika mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka 2018.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *