Mwanamuziki anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Nibebe’, Beka Flavour amefunguka na kusema kuwa Aslay siyo msanii mkubwa wa kumuangalia wakati anafanya kazi zake.

Beka amelazimika kusema hayo baada ya kuwepo minong’ono kuwa huenda anamuogopa msanii huyo ambaye zamani walikuwa wakifanya kazi pamoja kama kundi la ‘Yamoto Band’ kabla ya kila msanii kuanza kusimama mwenyewe.

Beka aliongeza kuwa “Aslay siyo msanii mkubwa kusema kwamba mimi nimuogope au nimfikirie. Hapa nchini msanii mkubwa ni Alikiba na ndo kama kioo najitazama lakini siyo Aslay. Mimi natazama wasanii wakubwa nje ya nchi lakini siyo ndugu yangu”.

Pamoja na hayo Beka amedai hataweza kumvumilia tena msanii huyo ambaye amefululiza kutoa nyimbo nyingi hivi karibuni endapo ataachia tena kazi mpya.

Pia amesema kuwa “Nimepanga kuachia wimbo mpya wiki mbili zijazo lakini kama Aslay akiachia tena kazi mpya sitaweza kumvumilia na mimi nitaachia mashine ili zipambane mbele kwa mbele maana mimi nimeshapanga ratiba zangu na siwezi kuzivunja,”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *