Mwanamuziki wa Bongo Flava, Beka Flavour kutoka Yamoto Band ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi nchini katika kituo cha Tabata Shule jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za utapeli wa mtandao.

Beka alishikiliwa kuanzia saa tano asubuhi baada ya kijana mmoja kuripoti kutapeliwa katika mtandao wa facebook kupitia jina la msanii huyo.

Baada ya kuachiwa kwa dhamana Beka alisema kuwa alipigiwa simu na polisi katika kituo cha Polisi cha Tabata Shule jijini Dar es Salaam akihitaji kufika hapo bila kukosa na msanii huyo akatii agizo hilo.

Beka aliendelea kusema kuwa baada ya kuripoti hapo akatiwa ndani akimsubili mshitaki ambapo baada ya kuwasili alikutanishwa nae kwa ajili ya mazungumzo.

Msanii huyo amesema kuwa mshtaki huyo amesema kuwa alikuwa anawasiliana na Beka kwa ajili ya kuunganishwa kwenye safari ya Yamoto Band kwenda nchini Marekani kwa hiyo akamtumia pesa Beka zaidi ya milioni nane ambapo Beka alikana kosa hilo.

Baada ya kupata dhamana Beka ametakiwa kuripoti kituoni hapo kila siku saa moja asubuhi mpaka upelelezi wa kesi hiyo utakapokamilika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *