Muigizaji wa Bongo movie, Bakari Makuka maarufu kama Beka jana alifanya sherehe ya harusi baada ya kufunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi.

Sherehe hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Prime Rose uliopo Mbezi Beach, Dar ikiwa ni baada ya kufunga ndoa na mkewe Nasra, Ijumaa iliyopita katika msikiti wa Ununio, Jumamosi ikafuatiwa na sherehe ya Maulid nyumbani kwao Beka, Sinza, Dar.

Baadhi ya wasanii wenzake walihudhuria kwenye sherehe hiyo ya harusi alikuwa Kulwa Kikumba ‘Dude’ pamoja na Dk. Cheni ambaye alikuwa mshehereshaji wa sherehe hiyo.

Jambo ambalo liliwashangaza baadhi ya wageni waalikwa waliuhudhuria kwenye sherehe hiyo kutokana na waigizaji wenzake kutojitokeza kwa wingi ili kumuunga mkono kwenye tukio hilo jambo ambalo siyo kawaida ya wasanii kutotokea kwenye shughuli kama hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *