Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Beka Ibrozama anatarajia kuzindua bendi yake ‘Spidoch Band’ katika ukumbi wa Next Door uliopo Masaki jijini Dar es Salaam Aprili 29 mwaka huu.

Beka amesema kuwa ametumia miaka mitatu kuandaa bendi hiyo ambapo alikuwa kimya kwenye game la muziki kutokana na maandalizi hayo.

Pia mwanamuziki huyo amesema kuwa amerudi tena kwa kushindo kwenye anga ya muziki kama alivyofanya nyuma wakati akiwa katika jumba la kukuza vipaji nchini THT akiwa na kina Barnaba, Amin na Lina.

Beka amedai alipokuwa nje ya muziki alipata nafasi ya kujifunza vitu mbalimbali ambavyo vitaboresha muziki wake kutokana na ukimya wake.

Aliongeza kwa kusema kuwa alipotea kwa muda mrefu kimuziki kwa kuwa aliamua kujitolea muda wake wote kwaajili ya kuandaa bendi yake.

Mwisho amewataka mashabiki wake kujitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi huo kwa ajili kuona wanamuziki wake wapya ndani ya bendi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *