Mwanamuziki wa Bongo fleva, Beka Ibrozama amesema kuwa anatarajia kufanya uzinduzi wa bendi yake itakayojulikana kwa jina ‘Spidoch Band’  ambapo maandalizi ya bendi hiyo yamekamilika kabisa.

Beka amesema kuwa bendi hiyo itakuwa bora kwani inawasanii wazuri na hivi karibuni wanatarajia kuachia nyimbo mpya ndani ya bendi hiyo.

Muimbaji huyo amesema amechukua muda mrefu kuiandaa bendi hiyo ili kukabiliana na ushindani uliyopo kwenye muziki wa bendi hapa nchini ila amesisitiza yupo tayari kukabiliana na ushindani uliopo.

Bendi hiyo inaingia kwenye orodha ya bendi zinazofanya muziki huo hapa nchini ambazo ni Yamoto Band, B- Band, Skylight Band na nyingine nyingi.

Beka Ibrozana ni mwanamuziki zao la Tanzania House of Talent (THT) ambaye amejizolea umaarufu kupitia kipaji chake cha uimbaji ambapo nyimbo zake zimebamba mashabiki wake mpaka kupelekea kufahamika zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *