Staa wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, klabu ya Man United na Real Madrid, David Beckham amepuuza uvumi unaodai kuwa ndoa yake inalindwa na brand ya ‘Beckham’.

Staa huyo aliyasema hayo wakati aliposhiriki kwenye kipindi kinachorushwa na idhaa ya BBC Radio 4 cha Derert Island Disc wakati kipindi hicho kikisherehea kutimiza miaka 75 ya kuanzishwa kwake.

‘Watu wanazungumza kuwa tuko pamoja kwasababu sisi ni brand? Bila shaka si hivyo’. Amesema Becks

‘Tuko pamoja kwasababu tunapendana. Tuko pamoja kwasababu tuna watoto wanne ‘amazing’.

Aliendelea kumwambia mtangazaji Kirsty Young kuwa: ‘Sisi ni familia imara. Tuna wazazi imara ambao wametulea kwenye malezi imara na sahihi.’

‘Ni kweli kuna wakati mnapitia magumu. Sote tunafahamu kuwa ndoa si jambo rahisi kunanyakati unafanya makosa lakini ni suala la kuyashughulikia hayo mkiwa pamoja’.

Kwenye kipindi hicho Becks alichagua ngoma ya Michael Jackson na Paul McCartney’s duet ‘The Girl Is Mine’ ambayop alii-dedicate kwa mtoto wake wa kike Harper.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *