Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Becka Title amesema kuwa wanamuziki wa kundi la B.O.B Micharazo hawajihusishi na utumiaji wala uuzaji wa dawa za kulevya.

Becka Title amesema hayo baada ya Mr Brue na Nyandu Tozy kutoka kundi hilo kutajwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wanahojihusisha na biashara ya kuelevya nchini.

Staa huyo amesema kuwa habari hizo ni za kizushi na zinasambazwa ili kuliaribia kundi hilo kutokea maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Beka amesema taarifa zilizopo mtanii kuwa baadhi ya wasanii kutoka kundi hilo wanauza na kutumia dawa za kulevya akiwemo Mra Blue ni uzushi usio na uhalisia wowote.

Mr Brue ni miongoni mwa wasanii waliotajwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya ambao wametakiwa kuripoti kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam lakini ameshindwa kuhudhuria kutokana na kutokuwepo nchini.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *