Mwanamuziki  mkongwe kutoka nchini Uganda, Bebe Cool amesema kuwa kituo cha runinga cha EATV kimefanya jambo kubwa kwa wasanii wa Afrika Mashariki baada ya kuanzisha tuzo za EATV.

Bebe Cool amesema tuzo hizo ni wazo zuri na pia ni jambo sahihi kwa wasanii kwa wakati huu, kwani hata kwenye siasa tayari wametambua umuhimu wa Afrika Mashariki .

Pia Bebe Cool amesema sasa ni takriban miaka 15 tangu itambulishwe East Africa Television na East Africa Radio na kutoa fursa ya muziki wa Afrika Mashariki kusikika hivyo ni kitu kikubwa kwao.

Tuzo za EATV zimeanzishwa na kituo cha runinga cha EATV na tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa katika ukumbi wa Mlimani City mwezi wa Disemba mwaka huu.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *