Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amemshukuru Gavana wa Mombasa, Hassan Joho kwa upendo anaomuonyesha.

Alikiba ametoa shukrani hizo kupitia akaunti yake ya Instagram ambapo amewaka picha pamoja na kuweka picha akiwa na Gavana huyo ndani ya Helkopta.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika  “My brother thank you for hosting me and my team in Mombasa. @joho_001 #KingKiba,”.

Kiba alikuwa miongoni mwa wasanii waliompigia kampeni Gavana huyo mpaka kupelekea kushinda kushinda ugavana kwenye uchaguzi wa Kenya uliofanyika August 8 mwaka huu.

Katika uhaguzi huo Joho aliwabwaga wagombea wengine akiwemo Awiti Bolo, Suleiman Shabahal na wengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *