Kiungo wa timu ya Manchester United, Bastian Schweinsteiger ameshinda tuzo ya heshima ya Special Jury kutokana na mchango wake aliowahi kuutoa kwenye timu yake ya taifa ya Ujerumani kabla ya kustaafu.
Kocha wa timu hiyo ya taifa, Joachim Low ameshinda tuzo hizo zilizoandaliwa na vyombo vya habari vya nchini Ujerumani ambazo hujulikana kwa jina la Bambi Awards.
Mchezaji huyo ambaye alikuwa kepteni wa timu hiyo ya taifa ya Ujerumani alitangaza kustaafu kuichezea timu hiyo mwezi Agosti mwaka huu.
Kiungo huyo ni miongoni mwa wachezaji waliofanikiwa kushinda kombe la dunia nchini Brazil baaada ya kuwafunga Argentina 1-0 katika dakika za ziada kwenye mechi hiyo.