Mbunge wa Nzega Mjini(CCM), Hussein Bashe amewataka wabunge wa CCM kuacha unafiki kuhusu suala la watekaji watu huku akisema kuwa yeye ni mmoja wa watu waliokamatwa na usalama wa Taifa.

Bashe ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu suala la utekwaji kwa watu lilianzishwa na mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.

CCM acheni unafiki mimi nimeshakamatwa na watu wa usalama mnasema hawakamati, kwa hili nipo tayari mniondoe kwenye chama”.

Bashe alikuja juu baada Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene kumtaka Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kuthibitisha kuwa matukio ya ukamataji yanafanywa na usalama wa Taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *