Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limesema kwamba baraza hilo limesikia tetesi ya bifu ilioyopo kati ya wanamuziki nyota wawili nchini Alikiba na Diamond na kama wakipelekewa mezani kuhusu suala hilo watalishughulikia.

Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza amesema amesikia kuna bifu kati ya Diamond na Alikiba lakini hawajapokea taarifa rasmi ambayo inayoonyesha mmoja kati yao akilalamika kuhusu mwenzie.

Mngereza amesema “Kwa upande wa serikali au BASATA tunafanya kazi kwa kuzingatia maandishi au taarifa rasmi, kwahiyo suala (la Alikiba na Diamond) halijatufikia rasmi,” alisema Mngereza. “Huu ni ushabiki au mashabiki ndio wanaleta haya, kwa hiyo ni ushabiki wa team hii na hii na tunaliona. Lakini kwa kuwa halijaja rasmi likija rasmi tutalishughulikia,”

Pia ameongeza kwa kusema kwamba “Lakini tukikutana na wao wenyewe wapo safi, kwa hiyo wanaosababisha hivyo ni mashabiki kwa sababu hata wachezaji wa Simba na Yanga wale ni wachezaji wapo kwenye tasnia moja, ni marafiki wanakaa pamoja, wanakula pamoja ni kama wanamichezo wa ngumi, wewe ukiwa nje unaangalia wao wanapigana kweli lakini ule ni mchezo. Kwahiyo mimi hii naona ni ushabiki wa mashabiki ambapo kimsingi huwezi kuwazua.

Diamond na Alikiba ni wasanii nyota wanaofanya vizuri kwasasa ndani na nje ya nchi lakini wamekuwa tofauti kutokana na mashabiki wao kugawanyika na kufanya wasanii hao kuwa na tofauti na wasiopikika chungu kimoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *