Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limesema wanaipitia video mpya ya Rich Mavoco na Diamond Platnumz ‘Kokoro’ ili kubaini kama kuna udhalilishaji wa wanawake na uvunjifu wa maadili.
Baraza hilo kupitia ukurasa wao wa Twitter wamedai kuwepo na thabiti katika kusimamia maadili na watatoa tamko kuhusu suala hilo muda si mrefu baada ya kuipitia.
Video hiyo imetoka jana na kupigwa kwenye vituo mbali mbali vya radio na runinga lakini imeonekana kukosa maadili baada ya wanawake kudhalilishwa kwenye video hiyo.