Hali ya kushangaza nchini Uingereza barua zilizoandikwa kwa mkono na Princess Diana zimeuzwa kwenye mnada uliofanyika jana siku ya Alhamis nchini humo.

Barua hizo sita zilitumwa kwa Cyril Dickman, aliyekuwa mwangalizi mkuu wa ikulu ya Buckingham miaka ya 1980 na 1990.

Katika barua moja iliyotumwa siku tano baada ya kuzaliwa kwa Harry, September 1984, Diana alimshukuru Dickman kwa kadi aliyomtumia na kueleza jinsi Prince William alivyokuwa anampenda mdogo wake huku barua hiyo ikiuzwa kwa paundi 3,200.

Diana alifariki kwa ajali ya gari mjini Paris nchini Ufaransa mwaka 1997 ameacha watoto wawili Prince William na Prince Harry.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *