Rais mpya wa Gambia, Adama Barrow anayetarajiwa kuwasili nchini mwake jioni ya leo, ameyaomba majeshi ya ECOWAS kussalia nchin humo kwa miezi sita zaidi.

Shirika la habari la AFP limedai kuwa afisa wa juu wa Umoja wa Mataifa barani Afrika, Mohammed Ibn Chambas amesema kuwa rais Barrow anataka kuhakikisha ulinzi na usalama nchini mwake unatengemaa kabla ya kusimamia dola yake mwenyewe.

Rais Barrow anayerejea akitokea Senegal alikokuwa kwa takribani mwezi mmoja kwa kuhofia usalama wake dhidi ya aliyekuwa rais wan chi hiyo, Yahya Jammeh.

‘Rais wa Gambia ameomba majeshi yaliyopo nchini mwake yabaki kwa miezi sita lakini huo ni uamuzi wa Ecowas’. Amenukuliwa Chambas

Barrow aliapishwa kushika wadhifa wa urais wiki iliyopita akiwa nchini Senegali wakati viongozi wa Ecowas walipokuwa wakimshawishi rais Jammeh ang’atuke madarakani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *