Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Elias Barnaba maarufu kama Barnaba Boy amesema kuwa hana mpango wa kufanya kolabo na msanii wa nje kwa sasa kwa kuwa bado anajipanga vizuri kisanaa.

Barnaba amesema kuwa si kwamba anaogopa ila kwa upande wake anaona bado anahitaji kujipanga zaidi ili atakapoamua kufanya kolabo yoyote iwe kubwa kama alivyorekodi na msanii wa Uganda, Jose Chameleone.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa “Muziki hautaki kubahatisha, mimi ni mwanamuziki ninayeongoza kwa kufanya shoo nyingi nje ya nchi, lakini sijataka kumshirikisha msanii yeyote wa nje kwa kuwa muziki wangu bado nauandaa, unaenda kidogo kidogo na nikiona umefika ninakotaka nitafanya hivyo,”.

Pia amemalizia kwa kusema kuwa kufanya hivyo hakumaanishi yeye ni msanii mdogo, ila katika maisha kila kitu lazima ufanye kwa malengo na baada ya wimbo wa ‘Love boy’ anatarajia kuachia wimbo wake mpya wa ‘Alone’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *