Staa wa Bongo fleva, Barnaba Classic amefunguka na kusema kuwa hivi karibuni atamtambulisha msanii mpya katika label yake ya High Table Sound baada ya kumsaini kwenye lebo hiyo.

Barnaba Boy amesema kuwa msanii huyo ni wa kiume anaitwa Mula na ndiye msanii wake wa kwanza kumsajili katika label yake na watu wategemee mengi kutoka kwa msanii huyo .

Staa huyo amesema “Ni kweli na msanii wangu wa kwanza ni wa kiume anaitwa Mula na hivi karibuni nitatoa kazi yake pamoja na video kabisa na itakuwa ni exclusive kabisa”.

Pia Barnaba ameongezea kwa kusema kuwa label yake ni kama shule ambayo inamsaidia msanii kujua vitu vingi ili aweze kufikia malengo yake katika sanaa ya muziki tofauti na lebo nyingine.

Barnaba anaungana na staa mwenzake Diamond Platnumz wanaomiliki lebo za muziki pamoja na wasanii wanaofanya kazi ndani ya lebo zao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *