Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barnaba amesema amemshukuru Mungu baada ya asubuhi ya leo kuletewa vitu vyake alivyoibiwa wiki iliyopita kwenye bahasha.

Barnaba amesema kuwa Mungu amemtendea miujiza baada ya kijana aliyejitambulisha kwa jina moja la John kumpatia bahasha iliyokuwa imetupwa ikiwa na vitu vyote muhimu alivyokuwa ameibiwa.

 Kupitia akaunti yake ya Instagram Barnaba ameandika kuwa “Amini msiamini Mungu yupo na ukitembea na Yesu hakuna linaloshindikana vitu vingine vimekosekana lakini hivi ni vikubwa zaidi nawashukuru wote mliopambana na kuniombea asante sana baba paroko kwa maombi mazito jana yametenda miujiza”.

 Pia ameongeza kwa kuandika “Na hiki kitabu huwa nakitumia sana kwenye ibada zangu za kila kukikucha hasa kwenye sala ya asubuhi jioni usiku pia na moja ya ulinzi wangu nacho kilikuwemo humo Mungu ametenda miujiza”.

Kutoa pesa katika vitu ambavyo vilikuwa vimeibiwa ni pamoja na kitabu cha chuo kidogo cha sala ambapo msanii huyo amesema ni kitabu anachokitumia mara kwa mara anapofanya ibada zake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *