Klabu ya Barcelona imemruhusu mshambuliaji wao, Neymar kujinga na PSG ya ufaransa kwa ada ya paundi milioni 198.

Raia huyo wa Brazil amewaambia wachezaji wenzake wakati wa mazoezi leo kuwa angependa kuondoka ndani ya klabu hiyo.

Alipewa ruhusa na meneja Ernesto Valvarde asifanye mazoezi na badala yake kushughulikia mpango wa uhamisho wake.

Mshambuliaji huyo ataruhusiwa kuondoka kwa gharama ya Euro milioni 222, ambazo PSG iko tayari kulipa.

Hatua hiyo inajiri siku mbili baada ya kubainika kwamba Barca ilikuwa tayari kuruhusu uchunguzi wa Fifa iwapo PSG ingemsajili Neymar.

Neymar alihamia Barcelona kutoka klabu ya Santos nchini Brazil 2013 kwa uhamisho wa pauni £46.6m na kusaini mkataba wa miaka mitano na mabingwa hao wa Uhispania 2016.

Neymar aliichezea klabu hiyo ya Barcelona katika mashindano ya ubingwa nchini Marekani kabla ya kusafiri kuelekea China ili kutimiza maswala yake ya kiamisho ndani ya klabu ya PSG.

Mchezaji huyo wa Barcelona aliifungia Barcelona mabao 105, kuisaidia kushinda mataji 2 ya ligi ,mataji 3 ya Copas del Rey na moja la vilabu bingwa Ulaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *