Klabu ya Barcelona imefikia  makubaliano ya kumsajili kiungo wa Brazil, Paulinho kutoka klabu ya Guangzhou Evergrande kwa ada ya paundi milioni 36.4.

Usajili huo utakuwa wa kwanza kwa Barcelona baada ya kumuuza mshambuliaji wake Neymar kwenda klabu ya Paris St-Germain.

Paulinho mwenye miaka 29 ambaye ni mchezaji wa zamani wa Tottenham anatajia kupima vipimo vya afya siku ya Alhamisi kwa ajili ya kukamilisha usaji huo.

Mchezaji huyo amejihakikishia namba kwenye timu ya taifa ya Brazili baada ya kuwasili kwa kocha Tite.

Tokea aanze kucheza timu ya taifa ya Brazil kiungo huyo ameshinda goli tisa katika mechi 41 alipoanza kucheza kuanzia mwaka 2011 pia alikuwepo kwenye kikosi kilichoshinda kombe la Mabara 2013.

Pia ameisadia timu yake ya sasa Evergrande kushinda taji la ligi kuu ya nchini China msimu uliopita kwa tofauti ya pointi tano na mshindi wa pili.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *