Klabu ya Barcelona imekamilisha usajili wa mshambualiji wa Borrusia Dortmund Ousmanne Dembele kwa uhamisho wa kitita cha paundi milioni 135.

Mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 20 amesaini mkataba wa miaka mitano katika uwanja wa Nou Camp akiwa na rais wa klabu hiyo Josep Maria Bartomeu jana.

Mkataba huo ni ya pili kwa thamani baada ya ile ya hivi karibuni ya Neymar kuelekea PSG iliogharimu pauni milioni 200.

Baada ya kusaini mkataba huo Dembele amesema kuwa anafurahia sana kujiunga na Barcelona kwa kipindi hiki kwani ni timu kubwa.

Mara ya mwisho kwa Dembele kuichezea Dortmund ni wakati wa kombe la Supercup mnamo tarehe 5 mwezi Agosti.

Klabu hiyo ya Bundesliga ilikataa ombi la Barca mapema mwezi Agosti , huku mchezaji huyo akiwa amepewa adhabu kwa kukosa mazoezi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *