Paris St-Germain leo watakuwa wenyeji wa Barcelona kwenye mechi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwenye uwanja wa Parc de Princes nchini Ufaransa.

Kiungo wa PSG alikuwa akisumbuliwa na majeraha Marco Veratt amepona na leo anatarajia kuwepo kwenye kikosi cha timu hiyo kwenye mechi hiyo dhidi ya Barcelona.

Kwa upande wa Barcelona, beki wa kati Gerard Pique anatarajiwa kucheza baada ya kukosa mchezo wa ligi kuu nchini Uhispania mwishoni mwa wiki dhidi ya Alaves.

Barca wataendelea kuikosa huduma ya beki wa pembeni Aleix Vidal ambaye alipatwa na majeraha ya kifundo cha mguu mwishoni mwa juma lililopita, na anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa miezi mitano.

Mchezo wa hii leo kati ya FC Barcelona na PSG, utakua unakumbushia mpambano wa wawili hao walipokutana katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya mwaka 2015, na Barca walifanikiwa kusonga mbele kwa jumla ya mabao 5-1, pia wababe hao wa Cataluña waliwahi kusonga mbele mwaka 2013 dhidi ya PSG kwa faida ya bao la ugenini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *