Klabu ya Juventus imeitoa Barcelona kwenye hatua ya robo fainali ya kombe la klabu bingwa Ulaya baada ya kutoka 0-0 kwenye mechi ya mkondo wa pili iliyochezwa kwenye uwanja wa Camp Nou.

Katika mechi ya kwanza iliyofanyika wiki iliyopita nchini Italia, Juventus ilishinda jumla ya goli 3-0 na kuwafanya kuwa faida ya kufuzu hatua ya nusu fainali.

Juve ambao mara ya mwisho kutwaa kombe hilo ilikuwa mwaka 1996 walionesha kiwango kizuri kwenye mechi ya jana baada ya kufaulu kuwakaba wachezaji hatari wa timu ya Barcelona, Neyma, Messi na Suarez.

Wachezaji wa Monaco, Mbape na Falcao wakishangilia moja ya goli kwenye mechi ya klabu bingwa jana dhidi ya Dortmund.
Wachezaji wa Monaco, Mbape na Falcao wakishangilia moja ya goli kwenye mechi ya klabu bingwa jana dhidi ya Dortmund.

Baada ya matokeo hayo, Juventus wanaungana na Real Madrid, Atletico Madrid na Monaco katika hatua ya nusu fainali ambapo droo itapangwa kesho.

Kwa upande mwingine Monaco nao imeingia hatua ya nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004 baada ya jana kuwabamiza Borussia Dortmund bao 3-1.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *