Klabu ya Barcelona inatarajia kumfikisha mahakamani aliyekuwa mshambuliaji wake Neymar kwa kutokana na madai ya kitita cha paundi milioni 7.8m kufuatia uhamisho wake katika klabu ya PSG.

Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Brazil alivunja rekodi ya uhamisho kwa kitita cha £200m kwa timu hiyo ya Ufaransa mnamo mwezi Agosti baada ya kununua mkataba wake katia klabu ya Barcelona .

Barcelona sasa inamtaka kurudisha marupurupu aliyopewa baada ya kutia saini mkataba mpya wa miaka mitano miezi tisa pekee kabla ya kulazimisha uhamisho huo.

Mbali na Euro milioni 8.5 za marupurupu, klabu hiyo pia inataka kulipwa asilimia 10 ya fedha hizo kwa kuchelewa kulipwa.

Barcelona pia inaitaka PSG kuchukua jukumu la kulipa fedha hizo iwapo mchezaji huyo atashindwa kulipa.

Kufuatia uhamisho huo Barcelona ilitangza kuwa inazuilia Euro milioni 26 za marupurupu ambazo mchezaji huyo alifaa kulipwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *