Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barakah The Prince amejitoa chini ya usimamizi wa lebo ya RockStar4000 aliyojiunga nayo mwaka jana.

Muimbaji huyo amesema kuondoka kwake hakuhusiani na Alikiba ambaye ni mmoja kati ya director wa label hiyo bali ni baadhi ya mambo na uongozi wa RockStar4000 hayajakaa sawa.

Baraka amesema kuwa“Sipo chini ya RockStar kwa sababau mimi ndio bosi wa muziki wangu, halafu mwisho wa siku mimi ndio nafanya kazi kwa hiyo kukiwa na vitu ambavyo haviko sawa kwa upande wangu naweza kutoa kauli ya mwisho.

Pia amesema kuwa kujitoa kwake hakuhusiani na Alikiba kuwa bosi wa kampuni hiyo ya muziki nchini.

Mwisho amemalizia kwa kusema kuwa kwasasa kazi zake zote zinasimamiwa na yeye mwenyewe chini ya kampuni yake ya Bana ambayo anamiliki yeye na mpenzi wake Naj.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *