Mwanamuziki wa Bongo fleva, Barakah The Prince ameonesha matunda aliyoyapata kutokana na muziki tangu aanze kuimba mwaka 2014.

Miongoni mwa mafanikio aliyopata ni pamoja na kujenga nyumba kubwa yenye vyumba 5 huku nje akiwa ameweka sehemu ya kuogelea (Swimming Pool).

baraka-mjengo

Baraka amesema kuwa yeye na mpenzi wake Naj wametumia fedha nyingi sana kwenye hiyo nyumba na bado haijakamilika na kwamba hayo ni matunda ambayo ameyapata kutokana na kazi ya muziki na ushirikiano na mpenzi wake huyo.

Hata hivyo msanii huyo aliongeza kwa kusema hivi karibuni anatarajia kufunga ndoa na penzi wake Naj baada tu ya kumaliza mjengo wake huo

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *