Mkali wa ‘Nisamehe’ Baraka The Prince amemporomoshea madongo ya kufa mtu rapa mtata nchini Nay wa Mitego baada ya rapa huyo kudai kwamba tofauti zilizopo kati ya Baraka na Stan Bakora ni kiki na wote anawaona kama watoto.

Nay wa Mitego amedai kuwa muimbaji huyo wa ‘Nisamehe’ na Stan Bakora ni watoto na kwamba huenda wanatafuta kiki.

Kutokana na kauli hiyo aliyoongea Nay wa Mitego imemtoa povu Baraka The Prince mpaka kupelekea kumwambia rapa huyo ana akili na kwasasa ana unga unga tu kutokana hana jipya kwasasa.

Baraka amesema kwamba  Nay wa Mitego ndio anaishi kwa makiki ndio maana mpaka alifungiwa kwa kupiga madada za watu picha za uchi huku akisisitiza sio mwanamuziki mzuri.

Pia Baraka The Prince ameongeza kwa kusema Nay wa Mitego ni rapper anayeungaunga, yaani huwezi kumweka miongoni kwa rappers wakali Bongo, huwezi kumtajia Nay wa Mitego nikakuambia kwamba ni rapper mkali.

Hayo yote yameibuka baada ya mchekeshaji maarufu wa vituko vya mkude Simba, Stan Bakora kufanya cover ya wimbo mpya wa Baraka The Prince aliyemshirikisha Alikiba ‘Nisamehe’ ambapo Baraka akupendezewa na namna Stan Bakora alivyoifanya nyimbo yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *