Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Baraka The Prince amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye hana tofauti yoyote na Alikiba na kudai kuwa watu wa mitandaoni ndiyo wamekuwa chanzo cha kusambaza maneno hayo kuonyesha yeye ana tofauti na Alikiba.

Baraka The Prince amedai kuwa yeye hawezi kugombana na Alikiba na wala hategemei kuja kumkosea kwa kuwa ni moja kati ya watu ambao wanampenda sana yeye pamoja na sanaa yake.

Mbali na hilo Baraka The Prince amesema kuwa mkali huyo wa Aje hivi sasa yupo kwenye maandalizi ya kuachia kazi yake mpya baada ya Aje kusumbua zaidi ya mwaka mzima.

Alikiba na Baraka The Prince licha ya kuwa chini la label moja ya  RockStar4000 wasanii hao pia waliachia kazi ya pamoja ambayo inafahamika kama ‘Nisamehe’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *