Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barakah The Prince amesema kuwa mahusiano yake ya kimapenzi na Naj bado yapo kama zamani licha ya kukaa kwa muda mrefu bila kuonekana pamoja.

Barakah amedai kuwa bado mapenzi yao yapo moto moto ila wameamua kutopenda sana kupostiana kwenye mitandao ya kijamii kama zamani.

Ameongeza kuwa ukurasa wake wa Instagram sasa utaendelea kujikita katika kazi zake zaidi na sio mambo ya uhusiano kama ilivokuwa zamani.

Wawili hao kwasasa hawapstiani kwenye mitandao ya kijamii kama ilivyokuwa zamani mpaka kupelekea kuibua mjadala kuwa wawili hao kwasasa hawapo pamoja lakini Baraka amekanusha taarifa hizo.

Baraka The Prince ambaye kwasasa anatamba na wimbo ‘Nisamehe’ aliomshirikisha Alikiba amesema kuwa mashabiki wake kama wanataka kuoana mahusiano yao kama zamani basi atacreate akaunti nyingine kuhusu mahusiao yake na Naj.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *