Mkali wa Bongo fleva, Barakah Da Prince amesema kuwa lugha ya Kingereza kwake ni tatizo kwahiyo anataka kutafuta mwalimu wa kumfundisha lugha hiyo.

Baraka Da Prince amesema katika interview yake kubwa iliyopita na MTV aliomba kutumia lugha ya Kiswahili kwa kuwa ndio lugha ambayo anaweza kuizungumza.

Pia muimbaji huyo amesema mpenzi wake wa sasa Naj ameshindwa kumfundisha kingereza na kuhamua kutafuta mwalimu yeye mwenyewe.

Muimbaji huyo ambaye kwasasa ameachia wimbo wake mpya ‘Nisamehe’ hivi karibuni akiwa amemshirikisha staa wa Bongo fleva, AliKiba ambaye pia wapo katika lebo moja ya Rockstar.

Baraka Da Prince ambaye kwasasa anafanya vizuri kwenye game la Bongo fleva ambapo amepata nafasi ya kuzunguka na tamasha la Fiesta linaloendelea katika mikoa tofauti hapa nchini.

Diamond Platnumz ni miongoni ya wasanii ambao walikuwa hawajaui kuongea lugha ya Kigereza hata kidogo lakini alijifunza na sasa anaongea kama kazaliwa Uingereza.

Wasanii wa Bongo fleva na Bongo movie wanapaswa kujifunza lugha ya kingereza ili kukuza kazi zao kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *