Beki wa Simba, Abdi Banda amemaliza adhabu yake na sasa yupo huru kuitumikia klabu yake ya Simba.

Mchezaji huyo alifungiwa na Bodi ya Ligi baada ya kumpiga ngumi mchezaji wa Kagera Sugar,  George Kavila.

Kamati ya nidhamu ilikaa na wakati inakaa tayari mchezaji huyo alikuwa amekosa mechi mbili hivyo kamati ilipitia  na kusikiliza pande zote mbili na kufanya maamuzi kuwa zile mechi mbili ambazo mchezaji huyo alizikosa ndiyo adhabu yake tosha kwa kosa alilofanya.

Awali mchezaji huyo baada ya kufanya tukio hilo ambalo mwamuzi hakuliona, alisimamishwa kucheza ligi kuu kusubiri maamuzi, na akakosa michezo dhidi ya Mbao FC na Toto Africans.

Mchezaji huyo wa Simba ataungana na wachezaji wengine wa klabu hiyo ambao wataingia kambini siku ya Jumapili kujiweka sawa dhidi ya mechi zilizobaki kwenye Ligi Kuu Bara ambazo zinaendelea nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *