Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imesema imeanza kupunguza maofisa walioko katika balozi na kuweka wapya ili kupanua wigo wa uwakilishi na kubana matumizi.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk Aziz Mlima wakati akizungumzia mambo mbalimbali yanayofanywa na wizara hiyo kwenye kipindi cha TUNATEKELEZA na kituo cha runinga cha TBC 1.

Mlima alisema kuwa ili kupanua wigo wa balozi katika kutangaza utalii nchini, waliamua kuwaondoa maofisa walioko kwenye balozi 35 na ofisi mbili za uwakilishi zilizopo nchi mbalimbali ili kupeleka watu wenye uwezo wa kutumia nafasi hiyo vyema.

Ameongeza kuwa lengo la kufanya hivyo ni kuongeza uwakilishi mzuri katika balozi hizo na kuboresha mazingira ya maofisa wao walioko nje kwa kutumia rasilimali chache zilizopo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *