Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youging ameipongeza bajeti iliyowasilishwa ya Serikali ya Tanzania kwa mwaka wa fedha 2017/18.

Bajeti hiyo imewasilishwa bungeni Mjini Dodoma juzi na waziri wa Fedha, Dkt. Philip Mpango.

Balozi huyo ameipongeza bajeti hiyo kwa kusema kuwa imeakisi dhamira ya kuongeza kasi ya maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu na viwanda.

Pamoja na hayo Dkt. Lu Youging amesema kwamba Tanzania ni sehemu ya kipaumbele cha China kwenye suala zima la uwekezaji na kwamba serikali yake itaendelea kushawishi wawekezaji wengi zaidi kuja kuwekeza nchini Tanzania ila kuchangia maendeleo na uzalishaji wa ajira nyingi zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *