Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga amesema Watanzania wengi wanashikiliwa katika magereza ya Afrika Kusini kwa makosa ya kujishughulisha na biashara ya dawa za kulevya.

Waziri Maiga sema hayo wakati akifafanua suala la Watanzania wanaoishi nje ya nchi hasa vijana na kusema wamekuwa wakijishughulisha na uuzaji dawa za kulevya badala ya kuwa raia wema.

Waziri huyo aliwataka kuacha kujishughulisha na mambo yanayoweza kuwaweka kwenye wakati mbaya na kutii sheria za nchi waliko.

Pia amesema Watanzania wengi waliopo Afrika Kusini wanafanya kazi ya kusafirisha dawa za kulevya katika mji wa Durban.

Waziri amesisitiza kwa kuseAma suala hilo ni moja ya mambo ambayo yamekuwa yakijadiliwa na Serikali ya Afrika Kusini ambapo Tanzania imejulishwa tatizo hilo na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Afrika Kusini pamoja na Rais Jacob Zuma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *