Aliyekuwa mgombea wa wadhifa wa mwenyekiti kutoka Kenya katika tume ya Umoja wa Afrika AU, Amina Mohammed ametaja usaliti miongoni mwa mataifa jirani ya Afrika Mashariki kuwa sababu ya yeye kutoshinda wadhfa huo.

Balozi Amina ambaye alipoteza wadhfa huo kwa mpinzani wake kutoka Chad Moussa Faki Mahamat alilaumu kushindwa kwake kulitokana na uwongo wa majirani za Kenya na siasa zinazoendelea kati ya mataifa yanayozungumza Kifaransa Francophone na wale wanaozungumza kizungu Anglophone.

Akiongea na vyombo vya habari vya kimataifa mjini Addis Ababa Amina alisema kuwa alipoteza wadhfa huo kutokana na usaliti wa majirani za Kenya ambao walikuwa wameunga mkono harakati zake.

Amina amesema kuwa “baadhi ya majirani zetu hawakutuunga mkono, walisikika wakizungumzia swala hilo Amina alisema bila ya kutaja majina.Nadhani hofu kwamba pengine Kenya ingeshinda ndio iliowafanya kutotuunga”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *