Kocha mkuu wa timu ya Liverpool Jurgen Klopp amemfukuza kwenye kikosi cha timu hiyo mshambuliaji wake, Mario Balotelli na kumruhusu kutafuta timu nyingine ya kujiunga nayo baada ya kushindwa kufikia kiwango cha kuridhisha kuweza kuchuana na washambuliaji wengine wa timu hiyo Daniel Sturridge, Divock Origi, Christian Benteke na Danny.

Balotelli ambaye ndio kwanza amerejea Liverpool akitokea AC Milan alikopelekwa kwa mkopo msimu uliopita amekutana na zahama hiyo muda mfupi uliopita.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Italia mwenye umri wa miaka 25, ameshindwa kupata mafanikio kwenye kikosi cha Liverpool tangu ajiunge nacho na amekifungia magoli manne tu kwenye mechi 28 alizoichezea timu hiyo tangu ajiunge nayo akitokea AC Milan mwaka 2014.

SUPER Mario Balotelli: WHY ALWAYS HIM?
SUPER Mario Balotelli: WHY ALWAYS HIM?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *