Mshambuliaji wa Nice, Mario Balotelli amesema kujiunga na Liverpool ulikuwa uamuzi mbaya zaidi aliowahi kuufanya maishani mwake.

Mshambuliaji huyo alifunga mabao manne katika mechi 28 alizochezea Liverpool baada ya kujiunga nao kutoka AC Milan mwaka 2014 kwa thamani ya paundi milioni 16.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amesema hayo kabla ya kufunga mabao mawili katika mechi yake ya kwanza na klabu ya Nice katika michuano ya Ligue 1 walipofunga mabao 3-2 dhidi ya Marseille siku ya Jumapili.

Meneja Brendan Rodgers, aliyemsajili Balotelli alifukuzwa na Liverpool mwezi Oktoba mwaka 2015, na Jurgen Klopp akachukua nafasi yake.

Baloteli kwasasa amehama Liverpool na kujinga na klabu ya Nice inayoshiriki ligi kuu nchini Ufaransa maarufu kama Ligi 1.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *