Mshambuliaji wa Nice, Mario Balotelli alitolewa nje ya uwanjani kwa mara ya tatu msimu huu baada ya kupewa kadi nyekundu kwenye mechi dhidi ya klabu ya Lorient katika Ligue 1.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool alitolewa uwanjani katika dakika ya 68 baada ya kumchezea vibaya ikabu Zargo Toure.

Bao la Wylan Cyprien, liliwapatia ushindi katika dakika ya 15 na kuwapatia ushindi wa kwanza katika mechi walizoshiriki ugenini tangu mwezi Novemba.

Nice wamesogea katika nafasi ya pili na alama tatu, nyuma ya Monaco, waliotoka sare ya 1-1 dhidi ya Bastia siku ya Ijumaa.

Balotelli , ameifungia klabu yake ya Nice magoli 11 tangu kuwasili kwake kutoka Liverpool msimu uliopita.

Balotelli alitolewa baada ya kupokea kadi mbili za manjano mara mbili katika mechi iliyopita dhidi ya Lorient mwezi Oktoba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *