Kiungo wa klabu ya Real Madrid, Gareth Bale leo anatarajia kurejewa uwanja kwenye mechi ya ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Napoli.

Bale mwenye umri wa miaka 27 amekuwa nje ya uwanja toka mwezi Novemba mwaka jana baada ya kuumia enka kwenye mechi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Sporting Lisborn ya Ureno.

Kwa upande wa kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema kuwa Bale atacheza kwenye mechi ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya Napoli leo kwenye uwanja wa Benabeu.

Naye kocha wa timu yake ya Taifa ya Wales Chris Coleman tayari amemjumuisha kiungo huyo kwenye kikosi cha timu hiyo kinachijiandaa kucheza mechi ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Jamhuri ya Ireland Machi 20 mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *