Winga wa klabu ya Real Madrid, Gareth Bale ameongeza mkaba mpya na klabu hiyo na kumfanya aendelee kudumu Bernabeu mpaka msimu wa mwaka 2022.

Bale mchezaji alijiunga na klabu hiyo akitokea Tottenham Hotspur ya Uingereza mnamo mwaka 2013.

Winga huyo kutokea Walese ameisaidia Madrid kushinda vikombe vitano katika misimu mitatu ya nyuma ikiwemo ligi ya mabingwa Ulaya mara 2 huku akifunga magoli 62 katika michezo 135.

Kabla ya Bale kusaini mkataba mpya wachezaji wawili wa timu hiyo Luka Modric na Toni Kroos nao pia walisaini mikataba mipya mwezi huu.

Mkataba wa Bale unatajwa kuwa wa Euro 600,000 kwa wiki huku baada ya makato ya kodi ikiwa Euro 350,000.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *